portal congregation p.m.s. urban college urban web site fides holy see
testata banner mongolia
 
 HOME ITALIANO ESPAÑOL ENGLISH FRANÇAIS PORTUGUÉS DEUTSCH CHINESE
Gospel
Saints
Papal Teaching
Congregation
Pontifical Mission Societies
Urban University
Mission texts
Animation
Statistics
From the Holy See
Testimonies
Martyrology
Jubilee 2000
Church life
Missionaries
Religious institutes
Movements & Associations
Catholic universities
Culture
History
Art
Cinema / Photo
Radio & tv
Music
Poetry
Health
Technology
Geography
News 360°
Dossier
In-depth study
Interviews
Stories
Book review
Children’s corner
Year 2005 World Mission Sunday Message in Swahili
UJUMBE WA BABA MTAKATIFU KUHUSU SIKU YA MISIONI DUNIANI
TAREHE 23 OKTOBA, 2005
DHAMIRA: “MISIONI: MKATE ULIOMEGWA KWA AJILI YA UHAI DUNIANI”
Wapendwa kaka na dada zangu,

1. Katika Jumapili ya Umisioni duniani, mwaka huu umetolewa ujumbe (Kaulimbiu) wa Ekaristi, unatusaidia kujua vizuri zaidi umaana wa Ekaristi katika maisha yetu, wakati tunaendelea kuishi dhamira ya Chumba cha Juu wakati katika undani wa mateso yake, Yesu alijitoa mwenyewe kwa Ulimwengu: “Usiku ule alipotolewa, alichukua mkate, na baada ya kushukuru, aliumega na kusema: huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili ya yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka: (1Kor. 11:23-24).

Katika barua yangu ya kichungaji ya hivi karibuni ‘Mane nobiscum Domine’, niliwaalika kutafakari juu ya Yesu katika “Kuumega Mkate” uliotolewa kwa ajili ya binadamu wote. Kwa kufuata mfano wake sisi nasi tunaitwa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu zetu na hasa wale wanaohitaji msaada wetu. Ekaristi ni “Ishara ya Umoja duniani” na kwa muono wa kisakramenti inaonyesha jinsi, “wote wanaoshiriki hali moja ya kibinadamu, waliozaliwa katika Kristo kwa njia ya Roho Mtakatifu na wanatwaa Utukufu wa Mungu, watakavyoweza kusema kwa pamoja: “Baba Yetu” (Ad Gentes 7). Kwa njia hii, wakati Ekaristi inasaidia kuelewa kikamilifu zaidi maana halisi ya MISIONI, inamwongoza kila muamini, kwa namna ya peke kila mmisionari, ili awe “Mkate, uliomegwa kwa ajili ya uhai wa dunia.”


2. UBINADAMU UNAMUHITAJI KRISTO “MKATE ULIOMEGWA”

Katika maisha yetu ya kila siku jamii ya kibinadamu inaonekana imefunikwa na dimbwi la vivuli vya giza wakati inatikiswa na matukio mazito yanayoleta uharibifu mkubwa wa mazingira katika dunia. Hata hivi kama vile “Usiku ule alipotolewa (1Kor. 11:23)” hata leo Yesu, “Anaumega Mkate.” (e.g. Mt. 26:26) kwa ajili yetu katika Ibada ya Ekaristi na anajitoa sadaka katika alama ya Sakramenti ya upendo wake kwa binadamu. Ndiyo maana nilieleza kwa msisitizo kwamba “Ekaristi si tu ni Ishara ya Umoja katika maisha ya kanisa, bali pia ni mfumo wa mshikamano wa wanadamu wote.” (Mane nobiscum Domine, 27; ni “Mkate kutoka Mbinguni” unaoleta uzima wa milele (cf. Jn. 6:33) na unauelekeza moyo wa mwanadamu kwenye tumaini kubwa zaidi.

Akiwa katika Ekaristia, Mkombozi yule yule aliyeona uhitaji wa kundi na akajaa moyo wa huruma “Kwa vile walikuwa wanateswa na kutupwa, kama kondoo wasio na mchungaji,” (Mt. 9:36) anaendelea katika karne (nyakati) kuonyesha upendo wa binadamu maskini na walio katika mateso.

Na ni katika jina lake ambapo wachungaji na wamisionari wanaeendelea kwenda sehemu ambazo bado hazijulikani kupeleka “Mkate” wa wokovu kwa wote. Wanasukumwa na ufahamu kuwa, muungano na Kristo “kiini si tu cha historia ya kanisa, bali pia cha historia ya ubinadamu (Ef. 1:10, Cal.1:15-20)” Mane naobisum Domine 6), inawezekana kuona kwa undani kabisa kiini cha moyo wa binadamu.

Yesu pekee ndiye anaweza kutosheleza mahitaji ya njaa ya Upendo na kiu ya Haki katika binadamu; ni yeye pekee anamfanya mwanadamu ashiriki katika maisha ya umilele: “Mimi ni mkate wa uzima ulioshuka duniani kutoka Mbinguni. Yeyote aulaye mkate huu ataishi milele” (Jn. 6:51)


3. KANISA, LILILO MOJA PAMOJA NA KRISTO, LINAKUWA “MKATE ULIOMEGWA”.

Wakati jumuiya ya Kanisa inaadhimisha Ekaristi na hasa Jumaipili, Siku ya Bwana, inagusa katika mwanga wa imani, thamani ya kukutana na Kirsto Mfufuka na kwa namna ya pekee inaelewa zaidi kwamba Sadaka ya Ekaristi ni kwa ajili ya wote (Mt. 26:28). Na sisi tunaoshiriki katika Mwili na Damu ya Bwana aliyesulibiwa na Kufufuka, hatuwezi kuiweka zawadi hii iwe kwa ajili yetu tu; kinyume chake, ni lazima tushirikishe. Upendo wa kisadaka kwa Kristo unatuongoza kumtangaza Kristo kwa ushujaa; ambapo kumtangaza huko katika ushahidi unakuwa ni sadaka kuu ya upeo katika kumpenda Mungu na Binadamu.

Ekaristi inatuongoza tuwe wainjilishaji wakarimu, wenye kujitoa kikamilifu katika kujenga ulimwengu wenye haki na udugu zaidi.

Kwa hakika natumaini mwaka wa Ekaristi utaiangaza kila jumuiya ya Kikristo kutoa jibu lenye “Mwamko wa Udugu katika baadhi ya namna nyingi za umaskini uliopo katika dunia yetu.” (Mane nobiscum Domine 28), kwa sababu “Kwa kupendana kwetu na kwa namna ya pekee kwa kuwajali zaidi wale walio katika shida zaidi, tutajulikana kuwa wafuasi kweli wa Kristo (Yoh. 13:35; Mt.25:31-46). Hiki kitakuwa ndicho kipimo cha kuhukumu ukanuni wetu katika kuadhimisha ibada zetu za Ekaristi.” (mane nobiscum Domine 28).


4. WAMISIONARI, “MKATE ULIOMEGWA” KWA AJILI YA UHAI WA ULIMWENGU.

Bado hata leo Kristo anawaambia wanafunzi wake: “Wapeni chochote cha kula ninyi wenyewe” (Mt. 14:16). Kwa jina lake wamisionari duniani kote wanatangaza na kushuhudia Injili. Kwa njia ya juhudi zao yanasikika tena maneno ya Mkombozi: “Mimi ni chakula cha Uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa; naye aniaminiye hataona kiu kamwe.” (Yoh. 6:35) nao wanakuwa pia “Mkate uliomegwa” kwa ajili ya ndugu zao, na wengine hadi kufikia kuutoa uhai wao.

Ni wamisoonari wangapi mashahidi katika nyakati zetu hizi! Tunatakia mfano huo uwaite vijana wengi wa kike na kiume kuthubutu kufuata njia ya ushujaa wa kiimani kwa Kristo! Kanisa linahitaji watu wake kwa waume kujitoa wakfu kikamilifu kwa ajili ya kuifuata njia kuu ya Injili.

JUMAPILI YA MISIONI ni wakati mwafaka wa kuongeza uelewo wetu juu ya umuhimu wa haraka wa kushiriki katika Utume wa Uinjilishaji katika jumuiya zetu na katika taasisi nyingi za kanisa na hasa vyama vya Kipapa vya Kimisionari na katika mashirika ya kimisionari.

Umisionari huu unahitaji msaada si tu wa Sala na sadaka, bali pia msaada wa mahitaji kamili. Natumia fursa hii kuwakumbusha bado juu ya uthamani na umuhimu wa huduma inayotolewa na Vyama vya Kipapa vya Kimisionari na nawaombeni nyote kuyachangia kwa ukarimu wote katika ushirikiano wa Kiroho na Kimahitaji.

Bikira Maria, Mama wa Mungu atusaidie kupunguza uzito wa Chumba cha Juu ili kwamba Jumuiya zetu za Kanisa ziwe za “Kikatoliki” zaidi, yaani ziwe jumuiya ambako “roho ya kimisionari” iliyoshikamana kwa undani na Kristo (Rm. 88), iwe karibu katika uhusiano wake katika “roho ya Ki-Ekaristi” ambapo Bikira Maria ni mfano, “Mwanamke wa Ekaristi.” (Ecclesia de Eucharistia 53); Jumuiya ambazo daima zipo tayari kwa kusikia sauti ya Roho na kwa mahitaji ya Ubinadamu, jumuiya ambapo waamini, na hasa wamisionari hawasiti kujitoa wao wenyewe kama, “Mkate, iliomegwa kwa ajili ya uhai wa Ulimwengu.”

Kwa wote natoa Baraka ya kichungaji.


Kutoka Vaticani, 22 February 2005, Sikukuu ya Ukulu wa Petro.

Yohane Paulo II

 
Index
Palazzo "de Propaganda Fide" - 00120 - Città del Vaticano Tel. +39-06-69880115 - Fax. +39-06-69880107 - e-mail: fides@fides.va © AGENZIA FIDES