portal congregation p.m.s. urban college urban web site fides holy see
testata banner mongolia
 
 HOME ITALIANO ESPAÑOL ENGLISH FRANÇAIS PORTUGUÉS DEUTSCH CHINESE
Gospel
Saints
Papal Teaching
Congregation
Pontifical Mission Societies
Urban University
Mission texts
Animation
Statistics
From the Holy See
Testimonies
Martyrology
Jubilee 2000
Church life
Missionaries
Religious institutes
Movements & Associations
Catholic universities
Culture
History
Art
Cinema / Photo
Radio & tv
Music
Poetry
Health
Technology
Geography
News 360°
Dossier
In-depth study
Interviews
Stories
Book review
Children’s corner
Year 2003 World Mission Sunday Message in Swahili
UJUMBE WA PAPA YOHANE PAULO II JUMAPILI YA UENEZAJI WA INJILI
19 OKTOBA 2003
Wapendwa kaka na dada zangu,
1. Tangu mwanzo wa utume wangu, nilipenda kuiweka kazi yangu ya Kipapa chini ya ulinzi maalumu wa Bikira Maria. Nimekuwa daima nikialika jumuiya yote ya waumini duniani kuishi ile hali waliyoishi wafuasi katika chumba "cha juu", ambako "waliishi katika sala pamoja na Maria, Mama wa Yesu" (Mdo 1:14). Katika hati yangu ya kwanza ya kipapa 'Redemptor hominis' (Wokovu wa watu wote), niliandika kwamba ni katika hali ya sala ya kina tu, tunaweza kupokea 'Roho Mtakatifu anayetujia na ndipo tunapokea ushuhuda wa Yesu Kristo hadi miisho ya dunia, kama wale waliokwenda kutoka kile chumba cha juu hadi Yerusalemu katika siku ya Pentekoste" (n. 22).

Kanisa linazidi kujitambua kuwa ni "Mama" kama alivyo Maria. Kama nilivyoonyesha wazi katika hati muujiza wa kujifanya mtu, katika kipindi cha kusheherekea Jubilei Kuu ya mwaka 2000, Kanisa ni hori ambapo Maria anamweka Yesu ili kumwonyesha awe kiini cha ibada na tafakari kwa watu wote. (N. 11). Kanisa linaamua kuendelea na njia hii ya kiroho na umisionari, likisindikizwa na Bikira Maria, Nyota wa Uinjilishaji mpya, kama taa na msaada wa uhakika katika hatua kwa hatua (cf. Novo Millenio Ineunte n. 58)

2. MARIA NA UMISIONARI WA KANISA KATIKA MWAKA WA ROSARI
Mwaka jana mwezi Oktoba, katika mwaka wangu wa 25 katika kazi yangu ya utume wa Petro, nilitangaza kuwa mwaka maalumu, kama mwendelezo wa roho ile ya Mwaka wa Jubilei, uwe ni mwaka wa kutafakari na kugundua zaidi juu ya sala ya Rozari, sala muhimu sana katika Utamaduni wa Kikristo! Ni mwaka tunaopaswa kuishi kwa kumfuata mmoja ambaye kwa mpango wa Mungu, pamoja na jibu lake la "Ndiyo", amewezesha wakovu kwa watu wote utendeke, na anaendelea kutoka mbinguni kuwalinda wale wote wanaomkimbilia, hasa wakati wa shida mbalimbali katika maisha yao.
Ningependa mwaka huu wa Rozari uwe muda mwafaka kwa waumini katika makontinenti yote, kuingia kwa undani zaidi ili kuelewa vema maana ya wito wao wa Ukristo. Kwa njia ya shule hii ya Bikira Maria na kwa mfano wa maisha yake, ni vyema kwamba kila jumuiya itatokea kwa vizuri zaidi kuwa na namna itakayoiwezesha kutafakari na kuingia zaidi katika Umisionari.

Iwapo Jumapili ya Uenezaji wa Injili, ambayo itafikia siku za mwisho za mwaka umaalumu wa Maria, itaandaliwa vizuri, italeta kiu kubwa ya moyo wa kujituma katika jumuiya ya kanisa. Makimbilio yetu kwa Bikira Maria, pamoja na kusali Rozari kila siku na pia kutafakari mafumbo ya maisha ya Kristo, yatahamasisha kuwa kazi ya Kanisa lazima itegemezwe kwanza kabisa kwa njia ya sala. Tabia ya "kusikiliza", ambayo inafanywa kwa njia ya kusali Rozari, inampeleka waumini awe karibu sana na Bikira Maria, ambaye "aliyaweka mambo yote haya, akiyatafakari moyoni mwake". (Lk. 1:19). Tendo la kutafakari mara kwa mara Neno la Mungu hutufanya tuishi, "Katika umoja na Yesu kwa njia (twaweza kusema) ya moyo wa Mama peke yake" (Rozarium Virginis).

3. KANISA LINALOTAFAKARI ZAIDI: SURA YA KRISTO
ALIYETAFAKARIWA:
Cum Mariae Contemplemur Christ Vultum!
Maneno haya hunijia mara nyingi akilini. Tafakari "Sura" ya Kristo pamoja na Maria. Tunapozungumzia "Sura" ya Kristo, tunazungumzia juu ya kufanana kwake na binadamu, ambapo utukufu wa milele wa mwana pekee wa Baba unang'ara juu yake (angalia Yoh. 1:14): "Utukufu wa Mungu kama kichwa unang'ara kutoka katika Sura ya Kristo". (RVM - 21). Kuitafakari Sura ya Kristo kunapelekea katika undani wa kina, undani wa kidugu katika fumbo lake. Kumtafakari Yesu kwa macho ya imani kunamfanya mtu apenye hadi katika fumbo la Utatu Mtakatifu wa Mungu. Yesu anasema. "Yeye aliyeniona mimi amemwona Baba." (Yoh. 14:9). Kwa njia ya Rozari tunasonga mbele zaidi katika safari ya fumbo hili, "pamoja na katika shule ya Mtakatifu sana Mama yake, (RVM - 3). Hakika, Maria anajifanya yeye mwenyewe kuwa mwalimu na mlinzi wetu.

Kwa njia ya Roho Mtakatifu anatusaidia tuwe na huo utulivu katika ulinzi huo unaowafanya waumini wasambaze imani yao kwa njia ya uzoefu wao katika Yesu na kwamba ni tumaini linalowahamasisha (RM - 24). Tumwone daima Maria, kama modeli asiye na mfano wa kulinganishwa. Maandiko yote ya Injili yanapata umaana usio kifani katika nafsi yake.

Bikira Maria ni kumbukumbu ya tafakari ya Kanisa liishilo na hamu ya kuunganika katika undani wake na Bibi harusi wake, ili kuwa na uhusiano wa ndani zaidi katika jamii yetu.

Je, tunajimudu vipi katika matatizo makubwa, katika mateso yasiyo ya haki, ukosefu wa haki aliingia kwa kiburi? Katika shule tulivu ya Maria Mama yetu, waumini wanajifunza kumtambua katika "ukimya wa Mungu unaojitokeza", Neno anayetenda katika ukimya kwa ajili ya wokovu wetu.

4. Kwa njia ya Ubatizo waumini wote wanaalikwa kwenye Utakatifu. Katika kanuni ya mwongozo 'Lumen Gentium', Mtaguso Mkuu wa II unasisitiza kuwa wito huo kwa jumla unatokana na wito wa wote kuelekea ukamilifu wa upendo.

Utakatifu na Umisionari ni maswala yasiyoweza kutenganishwa kuhusu wito wa kila mbatizwa. Hali ya kujitoa na kuwa Mtakatifu zaidi inaenda sambamba na ile ya kutawanya ujumbe wa wokovu. Katika Redemptoris Missio, nilikumbusha kuwa "Kila mmoja katika jumuiya ya waumini anaalikwa kwenye Utakatifu na Umisionari". (N.90). Katika kutafakari mafumbo ya Rozari, muumini anahamasishwa kumfuata Kristo na kushirikisha maisha yake, hivyo anaweza kuyarudia maneno ya Mtakatifu Paulo yasemayo "Siyo mimi niishiye bali ni Kristo aishiye ndani mwangu" (Gal. 2:20).

Iwapo mafumbo ya Rozari yanaunda shule muhimu ya kuelekea Utakatifu na Uinjilishaji, basi Mafumbo ya Mwanga yanarahisisha kwa namna fulani juu ya kuielewa vyema Injili, "Sequela".

Ubatizo wa Yesu katika mto Yordani unatukumbusha kwamba waliobatizwa, wameteuliwa kuwa "Waana wa Mwana" (Ef. 1:5; Gaudium et Spe N. 22).

Katika harusi ya Cana, Maria anawaalika wafuasi kumsikiliza kwa utii Neno wa Bwana: "Fanyeni lolote analowaambia" (Yoh. 2:5). Kutangazwa kwa Ufalme wa Mungu na waliko wa kutubu ni alama wazi ya Utume wa kila mmoja kuelekea Utakatifu.

Katika kubadilika Sura kwa Yesu, mbatizwa anaonja furaha inayomngoja baadaye. Katika kutafakari kuwekwa kwa Ekaristi Takatifu, mbatizwa anarudishwa kila mara katika "Chumba cha Juu", ambako Bwana aliwaachia Mitume wake utajiri mkuu kuliko wote: Yeye mwenyewe katika Sakramenti ya Altare. Kwa namna nyingine, ni yale maneno ambayo Bikira Maria aliyatamka pale Cana ndiyo yanajenga kumbukumbu ya Bikira Maria katika mafumbo yote ya Mwanga.

Hakika kumtangazwa kuwa Ufalme wa Mungu umefika, mwaliko kwa toba na huruma, kubadilika Sura mlimani Tabor na kuwekwa kwa Ekaristi Takatifu yanapata mwangwi maalumu katika Moyo wa Bikira Maria. Maria anayaelekeza macho yake kwa Kristo, anahifadhi kila neno, anatuonyesha jinsi ya kuwa wanafunzi halisi wa Mwanae.

5. KANISA LA KIMISIONARI ZAIDI: KUTANGAZWA KWA SURA YA KRISTO:
Haijawahi kutokea Kanisa likawa namna nyingi za kumtangaza Yesu kama sasa, shukrani nyingi kwa maendeleo ya teknolojia ya vyombo vya mawasiliano katika jamii. Kwa maana hiyo Kanisa la leo linaalikwa kuhakikisha kuwa Sura ya bibi harusi (Kanisa) inang'ara na kupendeza zaidi katika Utakatifu wake. Katika hili, kwa urahisi tu Kanisa linajua kuwa linasimamiwa na Mama Maria. Kwa njia ya Maria, "Linajifunza" kuwa "Bikira", anayejitoa kikamilifu kwa Bwana harusi wake, Yesu Kristo, na kwamba "Mama" wa watoto wengi ambao anawaelekeza kwenye uzima wa milele.

Chini ya uangalifu mkubwa wa Mama yake, jumuiya ya kanisa inashamiri kama familia iliyoimarishwa na mmiminiko mkubwa wa nguvu ya Roho, na inayopokea na kukubali mapokeo mapya ya Unjilishaji, inatafakari sura yenye huruma ya Yesu katika ndugu, hasa katika wale maskini na wahitaji, katika wale walio nyuma katika imani na elimu ya Injili. Kwa namna ya pekee, Kanisa haliogopi kuuhubiria ulimwengu kwa nguvu zote kuwa Kristo "ni njia, ukweli na Uhai" (Yoh. 14:6). Haliogopi kutangaza kwa furaha kuhusu "Habari njema, yenye nafsi Yesu Kristo kama kiini na roho, Neno aliyefanywa mwili, mkombozi pekee wa ulimwengu" (Rosarium Virginis Mariae - N. 20).

Ni vyema kuwaandaa wainjilishaji wenye uwezo wa walio wa Watakatifu. Utendaji wa roho ya mitume unatakiwa usipungue nguvu hata kidogo hasa katika swala la Utume kwa watu (umisionari ad gentes). Rozari ikigundulika vizuri na kupendwa ni namna tena ya kawaida izaayo matunda mema katika kuelimisha na ni chombo cha kiroho kwa ajili ya kuwafanya Taifa la Mungu kufanya kazi katika uwanja mpana katika shughuli za Kichungaji.

6. UTUME (MAHSUSI)
Kazi ya uongozi wa kimisonari lazima uendelee kuwa mathubuti, wajibu dhahiri kwa kila mbatizwa na jumuiya yoyote ya Kanisa. Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari, ni wazi yana kazi dhahiri na ya pekee, na ninayashukuru kwa kutenda jukumu hilo kwa ukarimu wote. Napenda kutoa wazo kwenu nyote kwamba iwapo jitahidini kuimarisha sala ya Rozari, binafsi na katika jumuiya, ili kupata kutoka kwa Bwana zile neema ambazo Kanisa na wanadamu wote kwa kweli wanahitaji. Namwaalika kila mmoja kufanya hivyo: Watoto, watu wazima, vijana na wazee, familia, maparokia na jumuiya za watawa.

Kati ya nia nyingi singependa kusahau ile ya kuomba Amani. Vita na hujuma vina kiini chake katika moyo "aliogawanyika." Kila mmoja anayetafakari juu ya fumbo la Kristo - na hii ni dhahiri lengo la Rozari - hujifunza siri ya Amani na anaifanya kuwa ni mradi wake. (RVM - N. 40).

Iwapo Rozari inajenga amani katika kasi ya maisha yetu, kinaweza kuwa ni chombo mahsusi kilichopendelewa kwa ajili ya kujenga amani ndani ya mioyo ya watu. Katika familia na kati ya watu. Pamoja na Maria, tunaweza kupata chochote tuombacho kutoka kwa mwanae Yesu. Kwa msaada wa Maria, hatutasita kujitoa kwa ukarimu katika kutangaza Habari Njema hadi miisho ya dunia.

Katika mawazo haya, kwa upendo mkubwa nawabariki nyote.

Imetolewa:
Vatican, 12 Januari, 2003
Sikukuu ya Ubatizo wa Bwana.
IOANNES PAULUS II

 
Index
Palazzo "de Propaganda Fide" - 00120 - Città del Vaticano Tel. +39-06-69880115 - Fax. +39-06-69880107 - e-mail: fides@fides.va © AGENZIA FIDES